Wakazi wa kijiji cha Matandalani kata ya Stalike Mkoani Katavi wameiomba serikali kuwatengea maeneo kwajili ya makazi na kilimo kutokana na adha wanayopata baada ya kuondolewa katika eneo la hifadhi.
Wamebainisha hayo
wakati wakizungumza na Mpanda fm na kusema hali ya maisha kwa sasa sio nzuri
kutokana na kutofanya shughuli za kilimo ambazo zimekuwa zikiwawezesha kuishi
salama.
Mjumbe wa Serikali za Mitaa katika eneo hilo amesema hata uongozi
umeingia dosari kutokana na watu kuwa wengi na wasiojua hatma ya maisha yao
baada ya kutofanya shughuli hizo za kilimo.
Wakazi wa eneo la
makutanio waliondolewa na serikali katika kijji hicho na kwa sasa wengi wao
wako katika kijiji cha Matandalani wakijaribu kufanya shughuri za machimbo ili
kupata mahitaji ya chakula.
Chanzo:
Ester Baraka
No comments:
Post a Comment