Baadhi ya
wafanyabiashara katika Halmashauri ya Manispaa
ya Mpanda mkoani Katavi wamesema kauli
ya waziri mkuu kwa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) itawasaidia kufanya biashara zao katika
mazingira mazuri tofauti na hapo awali.
Wameyasema hayo wakati
wakizungumza na Mpanda Redio kwa nyakati tofauti ambapo wameeleza kuwa hapo
awali TRA walikuwa wanatumia nguvu na lugha ambazo si rafiki kwao wakati
wakikusanya kodi hivyo kuleta kero katika shughuli zao za kibiashara.
Hata hivyo wameiomba
serikali kuweka msisitizo kwa TRA ili waweze kuongeza nguvu katika kutoa elimu
juu ya mlipa kodi ili kila mfanyabiashara aweze kupata elimu hiyo ambayo
itarahisisha ukusanyaji wa kodi.
Siku ya jana katika
kipindi cha maswali bungeni Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameionya Mamlaka ya
Mapato Tanzania (TRA) kutokutumia lugha za kuudhi wanapokwenda kudai kodi kwa
wafanyabishara huku akionya hatua zitachukuliwa kwa wenye tabia hizo.
No comments:
Post a Comment