Matukio ya utekaji wanahabari, kuibuka kundi la watu
wasiojulikana, kufungiwa vyombo vya habari na kupigwa faini kwa vyombo hivyo
vimetajwa kudunisha uhuru wa habari nchini.
Mwenyekiti wa Vyombo vya habari kusini mwa Afrika, tawi la Tanzania, (Misa- Tan) Salome Kitomari
Wakisoma hotuba zao leo
Mei 3 katika maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya
habari, Mwenyekiti wa Vyombo vya habari kusini mwa Afrika, tawi la
Tanzania, (Misa- Tan) Salome Kitomari amesema ni muhimu hatua zichukuliwe
kukabiliana na hali iliyopo sasa.
Kitomari amesema,
takwimu za taasisi kama waandishi wasio na mipaka na kamati ya
kulinda waandishi wa habari zinaonesha kushuka viwango vya uhuru wa
habari na kujieleza Tanzania.
Amesema mwaka jana
zimeripotiwa kesi za kupotea kwa waandishi wa habari, manyanyaso na
ukiukwaji wa uhuru wa vyombo vya habari.
Amesema wahabari
wanaitaka Serikali kupitia jeshi la polisi kuwatafuta waliohusika na kitendo
hicho na kuwachukulia hatua za kisheria.
Kaimu Mwenyekiti
wa Jukwaa la Wahariri, (TEF) Deodatus Balile amesema mazingira ya
kazi ya kuandika habari yamekuwa magumu kutokana na baadhi ya watendaji
wa vyombo vya dola kubugudhi na kuwafanyia uonevu wanahabari, huku kukiibuka
kundi la watu wasiojulikana.
No comments:
Post a Comment