Na Mwandishi Wetu
Wanawake wawili wilayani
Igunga mkoani Tabora wameuwawa kikatili kwa kukatwa na mapanga na watu
wasiojulikana huku mmoja akikatwa kiganja cha Mkono.
Mtendaji wa kata ya
Tambalale Salum Kitindi amesema kuwa aliyeuwa ni Elizabeth Charles mkulima wa
kijiji cha tambalale Tarafa ya Nsimbo, ambaye watu hao walimvamia usiku na
kumshambulia kwa mapanga hadi kupoteza uhai wake kasha kukata kiganja cha mkono
na kuondoka nacho.
Katika tukio linguine,
Mtendaji wa Kata ya Mwisi Issa Omary amemtaja aliyeuawa kuwa ni Suzana Alex,
mkazi wa kijij cha Busomeke, aliyeshambuliwa na mapanga huku mume wake John
Matheo akijeruhiwa na amelazwa Katika Hospitali ya Misheniya Ndala, Nzenga.
Mkuu wa wilaya ya Igunga
John Mwaipopo ambaye ni mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalam wa wilaya
amethibitisha Kutokea kwa matukio hayo na kueleza kuwa Jeshi la Polisi Igunga
Linaendelea na msako kuwabaini waliohusika.
Mkuu hyo wa wilaya ametoa
onyo kwa wanaojihusisha na vitendo vya uvunjifu wa sheria na Amani kuacha mara
Moja.
No comments:
Post a Comment