Waziri wa
Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu amesema
kufuatia kupatikana kwa taarifa ya ugonjwa wa Ebola huko DRC Congo hakuna
mgonjwa yeyote aliyehisiwa au kuthibitishwa kuwa na virusi vya Ebola hapa
nchini hadi wakati huu.
waziri Ummy Mwalimu |
Akizungumza
na vyombo vya habari leo, Mwalimu alisema nchi yetu inapakana na Jamhuri ya
Kidemokrasia ya Kongo, hata hivyo kuna uwezekano wa ugonjwa huo kuingia hapa
nchini kutokana na mwingiliano wa watu, hasa wasafiri wanaotoka na
kuingia.
Alisema
kutokana na hali hiyo wizara inaendelea kuchukua tahadhari ili kuzuia ugonjwa
huu usiingie hapa nchini.
"Wananchi
wanashauriwa kutokuwa na hofu, waendelee kuchukua tahadhari za kujikinga na
ugonjwa huu. Aidha Wizara inaendelea kusisitiza kuwa hadi sasa hakuna mtu
yeyote aliyethibitishwa kuwa na ugonjwa huu hapa nchini," alisema Ummy.
Vilevile
alisema wizara inaendelea kushirikiana na sekta mbalimbali katika kuimarisha
ufuatiliaji na kutekeleza mikakati ya kudhibiti ugonjwa huo ili usiingie hapa
nchini.
No comments:
Post a Comment