Na, Rehema Msigwa
SERIKALI
ya Mkoa wa Katavi imeweka bayana mpango
wake wa kuwasaidia watu wenye Ualbino, kupata vifaa mbali mbali kujikinga na
miali ya jua akiwemo matibabu.
Meza kuu wakifatilia jambo wakati wa maadhimo ya siku ya ualbino. |
Hayo
yamesemwa na mkuu wa wilaya ya Mpanda Lilian Charles Matinga katika maadhimisho
ya watu wenye Ualbino duniani yaliyofanyika katika uwanja wa Kashaulili uliopo
halmashauri ya Manispaa ya Mpanda kimkoa, ambapo ametumia muda huo kuikumbusha
jamii kuhusu usawa katika muktadha wa binadamu wote bila kujali mapungufu
waliyo nayo.
"watu wenye ualbino ni binadamu kama sisi, tena wengine wana uwezo kushinda hata sisi tunajiona ni wazima, tofauti yao na sisi ni rangi ya ngozi lakini hilo lisifanye sisi kuwaona hawafai,"Alisema Lilian
Baadhi ya waliohudhuria. |
Sanjari
na nasaha hizo amewataka wanganga wakienyeji wanao jihusisha na ramli
chonganishi kuacha mara moja kwani
mara kadhaa vifo vya watu wenye ualbino nchini Tanzania vimekuwa vikihusishwa
moja kwa moja na imani potofu zinazo sababishwa na waganga hao.
Kwa upande
wa Afisa maendeleo ya jamii Mkoa wa Katavi Anna Shumbi amesema kuwa idadi ya
watu wenye ualbino Mkoa wa Katavi ni 88
katika halmashauri tano ambapo idadi ya wanawake 41 na wanaume 47.
kwa upande wao baadhi ya watu wenye ualibino wameomba serikali kuendelea kuwawekea ulinzi na kuwasaidia katika mahitaji muhimu ikiwemo kofia za kujikinga na jua pamoja na mafuta maalumu ya kulinda ngozi zao.
"tunaomba serikali na wadau wengine watusaidie kofia, mafuta na kuendelea kutuimarishia ulinzi lakini serikali iendelee kuwaelimisha waganga wanaojihusisha na ramli kuacha ramli ambazo zinadhuru maisha yetu, sisi ni binadamu kama wengine hivyo jamii isituangalie tofauti." walisema wenye Ualibino
Kauli
Mbiu ni Takwimu na tafiti kwa ustawi wa watu wenye ualbino mkoa wa Katavi.
No comments:
Post a Comment