Wednesday, 14 June 2017

Wananchi wachangia Damu Katavi

 Na Alinanuswe
Baadhi ya wananchi mkoani Katavi wameonyesha kupokea kwa hamasa zoezi la uchangiaji damu linaloendelea katika hospitali ya wilaya iliyopo halmashauri ya Manispaa ya Mpanda ikiwa Leo ni siku ya uchangiaji damu Salama.
Baadhi ya wananchi waliojitokeza kuchangia wamesema kuwa uchangiaji damu unasaidia kuokoa maisha ya watu ambao wanahuitaji wakiwamo ndugu na jamaa.
"hii ni nafasi nzuri kwetu kuchangia, maana ukiwa na mgonjwa utapaswa tena kutafuta watu wa kuchangia damu bali utaonyesha ile fomu wanayokupa ambayo inakutambulisha kuwa wewe ni mchangiaji wa damu na unahudumiwa,"
"kwa kweli watanzania inabidi tuwe tunachangia damu hii itasaidia kupunguza vifo vya ndugu zetu, hata sisi kipindi tunapougua itatusaidia." Walieleza wachangiaji.
Mratibu wa damu salama mkoa wa Katavi Khadija Juma amesema kuwa uchangiaji wa damu husaidia kuokoa maisha hasa ya mama wenye matatizo wakati wa kujifungua, majeruhi wa ajali na wagonjwa wengine wenye uhitaji.
"watu wengi hulalamika pindi wanapoambiwa walete ndugu zao kuchangia damu lakini hiyo inatokana na upungufu wa damu, lakini kama watu wanaojitolea damu wangekuwa ni wengi basi mtu asingekuwa anaambiwa alete wa kujitolea damu"
kujitolea damu ni hiari lakini kwa mtu kufanya hivyo anaokoa maisha ya wengi wenye uhitaji, na kwa mwanaume anaweza kuchangia damu kila baada ya miezi mitatu na mwanamke ni kila baada ya miezi miwili," Alisema Khadija
Amesisitiza kuwa uchangiaji wa damu ni bure na ni hiari ufanyika kila baada ya miezi mitatu kwa mwanaume na miezi minne kwa mwanamke.
Ameongeza kuwa zoezi hili ni endelevu kwa wananchi kuchangia Changia damu, ambapo kauli mbiu ni “Changia Damu, Changia sasa, Changia mara kwa mara.”


No comments:

Featured post

MASIKINI WEEE!!!!! KICHANGA CHA SIKU MOJA CHAOKOTWA KATIKA KIWANJA CHA MPIRA AZIMIO

Na;Ezelina Yuda Mtoto mchanga mwenye jinsia ya Kike anayekadiriwa kuwa wa siku 1 ameokotwa akiwa hai kandokando ya uwanja wa azimio  ...