Saturday, 29 July 2017

Mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira MUWASA- Mpanda mkoani Katavi imeanza ujenzi wa mradi wa maji wa kanoge.

Mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira MUWASA- Mpanda imeanza ujenzi wa mradi wa maji wa kanoge ili kuongeza mita za ujazo 1,000,000 kwa siku ili kupunguza kero ya maji katika manispaa ya Mpanda katika mkoa wa katavi.

Hayo yamebainishwa na mkurugenzi wa mamlaka hiyo Injinia Zacharia Nyanda katika kikao cha nne cha baraza la madiwani wa halmashauri ya manispaa baada ya baadhi ya madiwani kusema kero ya maji imekuwa jambo kubwa katika maeneo yao.

 Ameongeza kuwa kuanzia mwezi wa kumi mwaka huu mamlaka itaanza ujenzi wa mradi wa maji wa ikolongo ii vilevile kutakua na ujenzi wa bomba la maji kutoka kazima hadi katikati ya mji. Aidha ameendelea kusema kuwa mamlaka itachimba visima kumi na moja kwenye maeneo ya manispaa amabyo yanashida ya maji na ambao mtandao wa mabomba haufiki.

 Maeneo mengi ndani ya manispaa ya mpanda bado yanakabiliwa na tatizo la maji ikiwemo kata ya makanyagio ambayo kwasasa wananchi wake hupata huduma ya maji kutoka katika nyumba za kulala wageni na katika visima vya watu binafsi.

No comments:

Featured post

MASIKINI WEEE!!!!! KICHANGA CHA SIKU MOJA CHAOKOTWA KATIKA KIWANJA CHA MPIRA AZIMIO

Na;Ezelina Yuda Mtoto mchanga mwenye jinsia ya Kike anayekadiriwa kuwa wa siku 1 ameokotwa akiwa hai kandokando ya uwanja wa azimio  ...