HARARE
Rais Robert Mugabe ameendelea kusisitiza
kuwa yeye ndiye kiongozi halali wa Zimbabwe na hataki kushiriki mazungumzo
yanayofanywa na Kasisi mmoja wa Kikatoliki ya kumuezesha rais huyo mwenye umri
wa miaka 93 kuondoka madarakani kwa amani baada ya mapinduzi ya kijeshi.
Duru ya kisiasa ambayo
ilizungumza na washirika wa ngazi ya juu waliowekwa katika kizuizi cha nyumbani
pamoja na Mugabe na mkewe, Grace, nyumbani kwa kiongozi huyo mjini Harare,
imesema Mugabe hana mipango ya kujiuzulu kwa hiari kabla ya uchaguzi unaopangwa
mwaka ujao.
Upinzani nchini humo
umemtaka Mugabe ajiuzulu maramoja na kuundwa haraka serikali ya mpito.
Katibu Mkuu wa chama cha MDC-T Change Morgan Tsvangirai
amesema wanaunga mkono hatua ya jeshi lakini nchi inapaswa kurejeshwa haraka
katika uongozi wa kikatiba.
No comments:
Post a Comment