Wednesday, 22 November 2017

Wafanya biashara wa vyakula katika soko kuu la Inyonga halimashauri ya wilaya ya Mlele mkoa wa Katavi Wameuomba uongozi wa halmashauri hiyo kuboresha miundombinu ya sokoni hilo.

Baadhi ya Wafanya biashara wa vyakula

 MLELE.

Wafanya biashara wa vyakula katika  soko kuu la Inyonga halimashauri ya wilaya ya Mlele  mkoa wa Katavi Wameuomba uongozi wa halmashauri hiyo kuboresha miundombinu ya sokoni hilo.

Wakizungumza na Mpanda Redio kwa nyakati tofauti wafanya biashara hao wamesema ili kuepukana na magonjwa ya mlipuko yanayoweza kujitokeza katika msimu wa mvua za masika ni vema wakashughulikia mapema suala hilo.

Hivi karibuni uongozi wa halimashauri hiyo umezindua mpango mkakati wa miaka mitano ambao utakuwa dira na mwongozo wa utekelezaji wa miradi ya maendeleo.

SOURCES:PAUL MATHIUS.

No comments:

Featured post

MASIKINI WEEE!!!!! KICHANGA CHA SIKU MOJA CHAOKOTWA KATIKA KIWANJA CHA MPIRA AZIMIO

Na;Ezelina Yuda Mtoto mchanga mwenye jinsia ya Kike anayekadiriwa kuwa wa siku 1 ameokotwa akiwa hai kandokando ya uwanja wa azimio  ...