Wednesday, 22 November 2017

Wananchi wa kata ya Mwamkulu iliyopo Manispaa ya Mpanda mkoani Katavi wameiomba serikali kuharakisha ujenzi wa kizibo cha maji ya umwagiliaji kabla ya msimu wa kilimo kuanza.



 

MPANDA.

Wananchi wa kata ya Mwamkulu iliyopo  Manispaa ya Mpanda mkoani Katavi wameiomba serikali kuharakisha ujenzi wa kizibo cha maji ya umwagiliaji kabla ya msimu wa kilimo kuanza.

Wakizungunguza na mpanda radio baadhi ya wakazi hao wamesema iwapo kizibo hicho kitakamilika watakuwa na uhakika wa kuvuna mavuno ya kutosha mwakani

Kwa upande wake diwani wa kata ya Mwamkulu Kalipi Katani amesema mradi huo tayari umeshatengewa bajeti lakini bado utekelezaji wake hauna mafanikio.

Mwaka jana serikali ilivunja kizibo cha asili kilichokuwa kinatumika na wakulima hao kuchepusha maji kuelekea kwenye mashamba yao kwa ahadi ya kuwa na njia mbadala ya kisasa ambayo haiathiri mazingira.

SOURCES:HARUNA JUMA.

No comments:

Featured post

MASIKINI WEEE!!!!! KICHANGA CHA SIKU MOJA CHAOKOTWA KATIKA KIWANJA CHA MPIRA AZIMIO

Na;Ezelina Yuda Mtoto mchanga mwenye jinsia ya Kike anayekadiriwa kuwa wa siku 1 ameokotwa akiwa hai kandokando ya uwanja wa azimio  ...