Baadhi ya
wafanyabisahara wa Mchele katika Halmashauri ya Mnispaa ya Mpanda wamesema
kubadilika haraka kwa bei ya mchele kunatokana na sababu mbalimbali ikiwemo
mwingiliano wa wafanyabiashara kutoka nje ya mkoa wa Katavi.
Wafanyabiashara hao
wamebainisha hali hiyo wakati wakizungumza na Mpanda Radio kuhusu hali ya
biashara ya mchele.
Hata hivyo
wamesema,wakati mwingine wafanyabiashara kutoka Kenya na Uganda hulazimika
kuchukua mchele kutoka Mpanda kutokana na ubora asili wa mchele unaopatikana.
Kwa sasa bei ya mchele
inatajwa kuwa kati ya shilingi 1000 mpaka 1400 kwa kilo.
No comments:
Post a Comment