Mkazi wa kata ya
Starike Tarafa ya Nsimbo mkoani Katavi
aliyefahamika kwa jina la Francis Aliseni Chapaulinge amehukumiwa miaka
ishirini jela kwa kosa la kupatikana na silaha kinyume cha sheria.
Tukio hilo lilitokea
tarehe 24 mwezi machi mwaka huu majira ya saa sita usiku ambapo mtuhumiwa
mwenye umri wa miaka 38 alikamatwa na bunduki moja aina ya SMG yenye namba
151614E na magazine moja isiyokuwa na risasi maeneo ya shambani kwake kijiji
cha Matandalani.
Hukumu hiyo imetolewa
tarehe 14 mwezi huu katika Mahakama ya
wilaya ya Mpanda mbele ya hakimu Chiganga Tengwa na Wakili wa serikali Hongera
Malifimbo na mtuhumiwa kukiri kutenda
kosa hilo.
Kumiliki silaha kinyume cha sheria ni kinyume na kifungu 20(b)na cha 2 cha sheria za
umiliki wa silaha za moto namba 2 ya mwaka 2015 kama ilivyofanyiwa marekebisho
mwaka 2006.
Chanzo:Furaha
kimondo
No comments:
Post a Comment