Mkuu
wa Wilaya ya Tanganyika Swalehe Mbwana Muhando amesema zoezi la
uandikishaji wa Vitambulisho vya Taifa
katika Wilaya yake linaendelea vizuri
japo kuna baadhi ya changamoto ziliweza kujitokeza.
Akizungumza
na Waandishi wa Habari amesema zoezi hilo limekumbwa na changamoto ya hali ya mvua kwa baadhi ya
maeneo hasa katika meneo ambayo miundombinu ni mibovu hali iliyopelekea Maafisa
wa Nida kushindwa kufanikisha zoezi hilo.
Aidha amewataka wananchi ambao bado
hawajaandikishwa kuendelea kusubiri
utaratibu ambao upo chini ya NIDA.
Zoezi
la uandikishaji wa vitambulisho vya Taifa linaendelea katika maeneo mbalimbali
Mkoa wa Katavi hivyo wananchi wametakiwa kujitokeza katika zoezi hilo.
No comments:
Post a Comment