Gari la Taka |
MPANDA
Wananchi katika manispaa ya
Mpanda mkoani katavi wamepongeza hatua ya manispaa kununua lori jipya la kubebea takataka.
Wakizungumza na mpanda Radio kwa nyakati tofauti wananchi hao wamesema kununuliwa kwa lori hilo kumekuja wakati muafaka hasa ikizingatiwa kulikuwa na uchafu uliokithiri katika maeneo mbalimbali.
Aidha wameitaka manispaa
kuhakikisha lori linaendelea kufanya kazi ili kuuweka mji wa mpanda safi.
Wiki iliyopita halmashauri ya
manispaa ya mpanda ilitangaza ununuzi wa lori jipya la kubebea taka lenye uwezo
wa kubeba tani 16 kwa zaidi ya shilingi milioni 159.
Chanzo:Haruna Juma
#Changia Damu Okoa Taifa
No comments:
Post a Comment