MOROGORO
Waziri wa Mambo ya Ndani ya
Nchi Dk Mwigulu Nchemba amewaagiza viongozi wa mkoa wa Morogoro kusimamia kazi
ya usajili na utambuzi wa watu kwa ajili ya kupewa vitambulisho vya Taifa.
Dk Nchemba ametoa agizo hilo
jana baada ya kuzindua kazi ya usajili na utambuzi inayofanywa na Mamlaka ya
Vitambulisho vya Taifa (NIDA).
Dk Nchemba amewataka viongozi
wakiwamo watendaji na wenyeviti wa Serikali za mitaa kuhakikisha hakuna mtu
ambaye si raia wa Tanzania anapewa kitambulisho.
Akisoma taarifa ya utendaji
kazi wa mamalaka hiyo, Kaimu mkurugezi Mkuu wa NIDA, Andrew Massawe alisema
tayari mashine 200 zimesambazwa ili kukidhi mahitaji ya usajili na kuhakikisha
ifikapo Aprili 30 mwaka huu kazi iwe imekamilika.
Kaimu mkurugenzi huyo ameitaja
mikoa ambayo imefanya vizuri katika kazi hiyo ya usajili na utambuzi kuwa ni
Iringa, Mara, Simiyu, Arusha, Geita, Mwanza, Ruvuma, Kilimanjaro na Lindi.
Chanzo:Mwanananchi
#Changia Damu Okoa Taifa
No comments:
Post a Comment