DAR ES SALAAM
Shirikisho la Vyama vya
Wafanyakazi Tanzania (Tucta) limeipongeza Serikali kwa uamuzi wa kulipa
malimbikizo ya madai ya watumishi wa umma wakiwamo walimu kwa kuwa itawaongezea
ari ya kufanya kazi.
Katibu Mkuu wa Tucta, Dk Yahaya
Msigwa amesema hatua hiyo itamaliza kilio cha muda mrefu cha wafanyakazi na
kuongeza ari ya kazi.
Hatua hiyo inakuja baada ya
serikali kusema malimbikizo ya madai ya watumishi wa umma 27,389 yenye thamani
ya Sh43.39 bilioni yatalipwa pamoja na mshahara wa Februari, 2018 kwa mkupuo.
Hivi karibuni Tucta
iliipelekea Serikali mapendekezo 11 yanayotakiwa kufanyiwa kazi kuboresha
mazingira ya wafanyakazi nchini ikiwamo malipo ya malimbikizo ya madai
yanayojumuisha madai ya watumishi ya zaidi ya miaka 10 iliyopita huku majina ya
watakaolipwa ikielezwa yanaanza kutangazwa kwenye vyombo vya habari.
Chanzo:Mwananchi
#Changia Damu Okoa Taifa
No comments:
Post a Comment