TANGANYIKA
Mkuu wa wilaya ya Taganyika mkoani Katavi Salehe Mhando amewataka
wananchi kuchagamkia fursa za uwekezaji katika mwambao wa ziwa Tanganyika.
Kauli hiyo ameitoa wakati wa
mahojiano na mpanda radio ambapo ameitaja wilaya hiyo kuwa utajiri wa misitu ya
utarii, ikiwemo masuala ya Uvuvi.
Katika hatua nyingine ameeleza
mikakati ya serikali kuwa ni pamoja na kuimarisha miundo mbinu itakayoenda
sambamba na ukuaji wa masuala ya kibiashara kati ya wilaya hiyo na wilaya
nyingine.
Wilaya ya Tanganyika inaumri wa mwaka
mmoja na nusu tangu kuanzishwa kwake huku ikitajwa kuwa kinara wa uzalishaji wa
mazao ya chakula kwa mkoa wa Katavi.
Chanzo:Alinanuswe Edward
#Changia Damu Okoa Taifa
No comments:
Post a Comment