![]() |
| Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari |
Friday, 16 February 2018
Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari amezindua ndege inayojiendesha yenyewe bila ya rubani.
ABUJA
Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari
amezindua ndege inayojiendesha yenyewe bila ya rubani ambayo ni ya kwanza
kutengenezwa nchini humo.
Kifaa hicho kilichotengenezwa na
Taasisi ya Teknolojia ya jeshi la anga la Nigeria, kitatumika kupambana na
wapiganaji pamoja na majambazi.
Mipango ya jeshi la nchi hiyo ni
kutengeneza vifaa hivyo kwa wingi na pia uwezekano wa kuvisafirisha katika nchi
nyingine.
Nigeria imekuwa ikikabiliwa na
kitisho cha usalama, ikiwemo wapiganaji wa kiislamu walioko kaskazini mwa nchi
hiyo, wapiganaji walioko katika eneo lenye utajiri wa mafuta, kusini mwa nchi
na mapigano kati ya wafugaji na wakulima katika jimbo la kati mwa nchi hiyo.
Source EATV
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Featured post
MASIKINI WEEE!!!!! KICHANGA CHA SIKU MOJA CHAOKOTWA KATIKA KIWANJA CHA MPIRA AZIMIO
Na;Ezelina Yuda Mtoto mchanga mwenye jinsia ya Kike anayekadiriwa kuwa wa siku 1 ameokotwa akiwa hai kandokando ya uwanja wa azimio ...
-
KATAVI Shule ya msingi Misunkumilo iliyopo Manispaa ya Mpanda mkoani Katavi inakabiliwa na uhaba wa vyumba vya madarasa na madawati...
-
KIGOMA . VITUO vya afya Uvinza na Nguruka vilivyopo wilayani Uvinza Mkoa wa Kigoma vinakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo yaup...
-
NSIMBO Soko la Katumba Mnyaki linalomilikiwa na halamshauri ya Wilaya ya Nsimbo Mkoani Katavi halina choo tangu kuanzishwa kwake hali...

No comments:
Post a Comment