MPANDA
Wazee wilayani Mpanda mkoa wa Katavi wameipongeza
serikali kwa kuimarisha huduma ya afya ikiwemo mpango wa matibabu bure kwa
wazee.
Katika mazungumzo na Mpanda radio fm wameelezea namna wanavyo pewa
kipaumbele tofauti na hapo awali ambapo iliwalazimu kubakia kwenye foleni
wakisubiri matibabu.
Dokta Jafari Kitambwa Mganga mkuu
wa Hospitali ya Manispaa ya Mpanda amesema kuwa huduma zote zinatolewa bure
kuanzia upimaji, matibabu na Upasuaji.
Pia amesema kuwa serikali imetenga wahudumu maalumu ambao wanahusika na
utoaji huduma kwa wazee ili kuwatenganisha na makundi mengine hospitalini
kuepusha msongamano wa wagonjwa.
No comments:
Post a Comment