Waziri Mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa
MWANZA
Madiwani
wa Halmashauri ya Buchosa wilayani Sengerema wamemuomba Waziri Mkuu Kassim
Majaliwa aondoke na Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, Bw. Cyprian Luanda baada ya
kutoridhishwa na utendaji wake.
Wametoa ombi hilo katika kikao cha Waziri Mkuu na
watumishi Halmashauri ya Buchosa akiwa katika siku ya kwanza ya ziara yake ya
kikazi mkoani Mwanza.
Waziri Mkuu baada ya kupokea ombi hilo amemuagiza
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Bw. John Mongella kwenda katika halmashauri hiyo na
kufanya kikao cha pamoja kati ya Madiwani, Mkurugenzi na watumishi ili kubaini
changamoto zilizopo na kuzitafutia ufumbuzi.
Mbali na hayo Mh. Majaliwa ameweka jiwe la msingi
la hospitali ya Halmashauri ya Buchosa wilayani Sengerema, ambapo ujenzi wake
hadi kukamilika unatarajiwa kugharimu sh. bilioni 10.55.
Pia Waziri Mkuu amezindua madarasa manne ya Kidato
cha Tano na Sita katika Shule ya Secondari ya Nyehunge wilayani Sengerema na
kuwataka wanafunzi wasome kwa bidii.
Chanzo:EATV
No comments:
Post a Comment