Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya manispaa ya Mpanda Bw. Michael Nzyungu |
Halmashauri
ya Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi imepata shilingi milioni 281 kwaajili ya
kutatua changamoto ya uhaba wa vyumba
vya mdarasa na maabala katika shule mbalimbali.
Kauli
hiyo imetolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri hiyo Michael
Nzyungu,wakati akizungumza na Mpanda Radio kuhusu tatizo la wanafunzi wa shule
ya sekondari Kasokola kusomea katika vyumba vya maabala vyenye kemikali hali inayo
hatarisha usalama wa walimu na wanafunzi.
Aidha
Nzyungu amekiri kuwa tatizo hilo limetokana na wingi wa wanafunzi katika shule
hiyo hususani kidato cha kwanza walioripoti mwaka huu.
Shule
ya sekondari Kasokola ina jumla ya wanafunzi 415 ambayo ni miongoni mwa shule
za sekondari 16 za manispaa ya Mpanda,tangu ianzishwe mwaka 2008 inakabiliwa na
uhaba wa walimu wa masomo ya sayansi.
Chanzo:Issack Gerlad
No comments:
Post a Comment