Wananchi wa mkoani katavi wakitoa maoni |
Wananchi wa mkoa wa katavi manispaa ya mpanda wametoa maoni yao kuhusu ukuaji wa uchumi nchini huku wakiilalamikia serikali kuwapandishia tozo za kodi kitu kinachopelekea kuua mtaji wa biashara.
Walisema kuwa
uchumi wa nchi unakua ingawa bado wanapata shida katika ulipaji kodi kutokana
na tozo hizo kupanda bei na biashara zao hazina mtaji mkubwa ‘serikali
inatakiwa kuangalia swala hili katika jicho la tatu kwa kuwa wafanyabiashara
wadogo tunashindwa kutumia mashine za EFD na huku mitaji ni michache’amesema
Charles Ruben mmoja wa wafanyabiashara.
Uchumi wa Tanzania umekuwa ukikua kila mwaka ambapo
mpaka kufikia mwaka2016 kiwango cha juu cha ukuaji wa uchumiumefikia
asilimia6.9 ikiwa imeshikilia nafasi ya pili katika nchi za bara la afrika
ikiongozwa na nchi ya Cote D’ivore ikiwa
na asilimia 8.5.
Chanzo:Ezelina Yuda
No comments:
Post a Comment