NSIMBO
Wananchi
wa Kata ya Kanoge halmashauri ya Nsimbo mkoani Katavi wameitaka halmashauri
hiyo kutoa maelezo juu ya utata wa tozo mbali mbali za mazao ya Kilimo.
Katika
mkutano wa hadhara uliofanyika katika soko la Kanoge wananchi wameituhumu wazi
wazi halmashauri hiyo kukiuka agizo la Rais wa Tanzania Dk John Pombe Magufuli
kuhusu kuachana na mpango wa kutoza ushuru mazao yasiyo zidi tani moja.
Katika
hatua nyingine wameelezea kukerwa na baadhi ya vitendo vya mawakala wa ushuru
katika mageti kuhatarisha usalama wao, kwa kuinua kamba kwa ghafla.
Mwenyekiti
wa halmashauri ya Nsimbo Raphael Kalinga amepiga marufuku kuwepo kwa ushuru
mdogo mdogo ambao haupo kisheria .
Chanzo:ALINANUSWE EDWARD
No comments:
Post a Comment