TANGANYIKA
Wananchi wa kijiji cha Kapanga kata ya Katuma
wilaya ya Tanganyika wametakiwa kuzingatia mpangilio na uboreshaji wa makazi
holela ili kuwasaidia wanafunzi ambao wamekuwa wakitembea umbali mrefu.
Hayo yamesemwa na Afisa mipango miji na
vijiji Elisha Mengele wakati akizungumza katika mkutano na wananchi wa kijiji hicho na kusema kuwa
makazi holela yamekuwa ni kikwazo katika sekta ya elimu kwani wanafunzi
wamekuwa wakitoka umbali mrefu hali inayopelekea kushuka kwa kiwango cha
ufaulu.
Naye mkuu wa Wilaya ya Tanganyika Saleh
Mbwana Muhando ametoa rai kwa wananchi ambao wanaishi mbali na huduma za
kijamii kuhamia katika maeneo ambayo serikali imetoa kwani hatua za kisheria
zitachukuliwa kwa wale ambao wanaishi katika makazi holela.
Kutokana na uwepo wa makazi holela wanafunzi
wanaosoma katika shule ya Msingi Kapanga wanalazimika kutembea umbali wa
kilomita 30 kila siku.
Chanzo:Restuta Nyondo
No comments:
Post a Comment