Thursday, 7 December 2017

Kijiji cha Mtambo kilichopo kata ya Katumba Wilayani Mpanda Mkoani Katavi,kimefanikiwa kutokomeza vifo vya akina mama na watoto.


NSIMBO
Kijiji cha Mtambo kilichopo kata ya Katumba Wilayani Mpanda Mkoani Katavi,kimefanikiwa kutokomeza vifo vya akina mama na watoto.
Hatua hiyo imethibitishwa na Katibu wa Kijiji cha Mtambo Bw.Fenias Fulujensi wakati akizungumza na Mpanda Radio kujibu malalamiko ya baadhi ya wananchi wanaolalamika kutozwa faini ya shilingi elfu ishirini kutoka kwa wananchi ambao wake zao wanaojifungulia nyumbani.
Bw.Fulujensi amesema katika kipindi cha mwaka 2016 mpaka 2017 wanawake watatu wamefariki dunia kutokana na kuchelewa kufika katika vituo vya huduma za afya ambapo kwa sasa hakuna ripoti ya vifo hivyo.
Hata hivyo hivyo Kamimu afisa mtendaji wa Kata ya Katumba Bi.Lucy Kagine ameunga mkono faini hiyo japo amesema hana taarifa ya uwepo wa faini hiyo katika kijiji hicho.
Kwa mjibu wa mwenyekiti wa Kamati ya zahanati ya Mtambo Bw.Karoli Shaltiel amesema kwa kushirikiana na Halmashauri ya serikali ya kijiji cha Mtambo wamechukua hatua ya kutunga sheria ndogondogo za kutoza faini baada ya kuonekana asilimia 60 ya akina mama wanajifungulia nyumani hali ambayo imesababisha vifo kwa mama na mtoto.

No comments:

Featured post

MASIKINI WEEE!!!!! KICHANGA CHA SIKU MOJA CHAOKOTWA KATIKA KIWANJA CHA MPIRA AZIMIO

Na;Ezelina Yuda Mtoto mchanga mwenye jinsia ya Kike anayekadiriwa kuwa wa siku 1 ameokotwa akiwa hai kandokando ya uwanja wa azimio  ...