Monday, 22 January 2018

SPD waridhia mazungumzo ya serikali ya muungano.



Außerordentlicher SPD-Parteitag Andrea Nahles und Martin Schulz umarmen sich (picture alliance/dpa/K. Nietfeld
)

Asilimia 56 ya wajumbe 642 wa chama cha Social Democrat SPD wameunga mkono mazungumzo ya kuunda serikali ya muungano pamoja na vyama ndugu vya kihafidhina CDU/CSU yaanze. Nini kitafuata baadae?
"Sote tumeshusha pumzi bila ya shaka. Ni matokeo yanayodhihirisha jinsi mapambano yalivyokuwa makali. Bila ya shaka nimefurahi kuona kwamba tumekabidhiwa jukumu la kuongoza mazungumzo ya kuunda serikali ya muungano."
Furaha yake si ya bure kwasababu pindi walio wengi wangepiga kura ya "la" basi uchaguzi mpya ungebidi uitishwe, na hakuna si Martin Schulz na wala si Angela Merkel, ambae angeachiwa kuongoza orodha ya wagombea wa chama chake.
Wana SPD waamua
 Vigogo wa SPD wapania kurejesha mshikamano chamani
Katika mahojiano na kituo cha televisheni cha Phoenix mara baada ya uamuzi huo kupitishwa, mwenyekiti wa chama cha SPD, Martin Schulz ameahidi kufanya kila liwezekanalo kurejesha mshikamano chamani baada ya mfarakano uliojitokeza katika mkutano mkuu wa dharura, jana mjini Bonn.
Bila ya kutilia maanani madai ya wapinzani wa serikali ya muungano wa vyama vikuu, makubaliano yatakayofikiwa, baada ya mazungumzo yanayoanza hii leo, huenda yakakataliwa wanachama wa SPD watakapoulizwa maoni yao. Kuna baadhi ya viongozi wa SPD wanaoonya dhidi ya kuvuta wakati katika mazungumzo ya kuunda serikali ya muungano. Maoni sawa na hayo yametolewa pia na kansela Angela Merkel anaesema:"Njia imeshafunguliwa ya kuanza mazungumzo ya kuundwa serikali ya muungano. Mwongozo ni makubaliano yaliyofikiwa katika mazungumzo ya awali. Na bila ya shaka kuna masuala mengi yatakayobidi kufafanuliwa. Na hayo pia atakuwa bila ya shaka majadiliano makali."


 Jusos wamepania kupinga serikali ya muungano wa vyama vikuu  GroKo
Mwenyekiti wa SPD, Martin Schulz sawa na viongozi  wengi wengine wa chama hicho wanatilia mkazo umuhimu wa  kutilia mkazo msimamo wa chama chao mazungumzoni na kuhakikisha mada muhimu zinazohusu masilahi ya jamii zinajumuishwa katika makubaliano ya mwisho. Wanachama cha SPD watatakiwa mwishoni mwa mazungumzo hayo yatakayoanza leo usiku kutamka kama wanakubaliana serikali iundwe au la.
Vijana wa SPD-JUSO, wanaopinga mtindo mmoja serikali ya muungano wa vyama vikuu GroKo, wanasema watafanya kampeni kote nchini ili kuwatanabahisha wanachama wasiunge mkono serikali ya muungano wa vyama vikuu GroKo.
Chanzo:Dw swahili.

No comments:

Featured post

MASIKINI WEEE!!!!! KICHANGA CHA SIKU MOJA CHAOKOTWA KATIKA KIWANJA CHA MPIRA AZIMIO

Na;Ezelina Yuda Mtoto mchanga mwenye jinsia ya Kike anayekadiriwa kuwa wa siku 1 ameokotwa akiwa hai kandokando ya uwanja wa azimio  ...