MPANDA
Wakazi
wa kijiji cha Dilif kata ya Magamba
wilayani Mpanda mkoa wa Katavi
wameilalamikia serikali kwa kutotatua kero ya maji inayowakabili kwa mda mrefu
katika kijiji hicho.
Wakizungumza na Mpanda Radio kwa Nyakati
tofauti wamesema afya zao zipo hatarini kutokana na kutumia maji kutoka vyanzo
vyenye maji machafu ikiwemo yatokanayo migodi inayo hofiwa kuwa na sumu
aina ya mekyuri.
Kwa upande wake diwani wa Kata hiyo Mh.Philipo Kalyalya amesema kisima kilichochimbwa kipo katika hatua za mwisho na amewataka wakazi kuwa wavumilivu wakati tatizo hilo likishughulikiwa.
Kijiji
cha Dirifu kina zaidi ya wakazi elfu
moja wanaoathirika kutokana na ukosefu wa huduma ya maji.
#Changia Damu okoa Taifa.
Chanzo:Neema Manyama
No comments:
Post a Comment