MPANDA
Baadhi
ya wafanyabiashara manispaa ya Mpanda
mkoani Katavi wamelishutumu shirika la umeme [Tanesco] kwa kutotoa taarifa kuhusu kukatwa
kwa umeme.
Wakizungumza
na mpanda redio na wameeleza kuwa tatizo
la kukatika kwa umeme mara kwa mara imekua ikisababisha kukwama kwa biashara
zao hasa zinazotegemea umeme hivyo kupelekea kukosa wateja na kushindwa
kujiingizia kipato.
Wafanya
biashara na watumiaji umeme majumbani wanataka mamlaka kujenga kasumba ya kutoa
taarifa kuhusu katizo lolote la umeme ili kuodoa usumbufu usio wa lazima.
Lakini msemaji wa Tanesco mkoani Katavi
ambaye amehojiwa kwa njia ya simu amedai
kuwa hana taarifa zozote kuhusiana na kukatika kwa umeme siku ya jana na usiku wa kuamkia leo.
Mkoa
wa Katavi ni miongoni mwa mikoa ambayo mpaka sasa inatumia majenereta kama
chanzo cha nishati ya Umeme.
No comments:
Post a Comment