KATAVI
Baadhi ya vikundi vya wachimbaji
wadogo wadogo wa madini mkoani Katavi wameilalamikia serikali kuchelewesha
mchakato wa kuwapatia leseni ili waweze kufanya shughuli zao kwa uhuru.
Wakizungumza na mpanda
Radio FM wanakikundi cha Kagera Group kutoka kijiji cha Dilifu Manispaa ya Mpanda
wamesema wameomba leseni tangu mwaka jana lakini kila wakifuatilia wamekuwa
wakipata majibu yasiyoridhisha
Akizungumza na Mpanda
radi ofisini kwake Kamishna msaidizi wa madini kanda ya magharibi Mhandisi
Sementa J. Haruna amesema kinachosababisha kuchelewa kutolewa kwa leseni kwa
wachimbaji hao kunatokana na kubadilishwa kwa sheria ambapo kwa sasa tume ya
madini ndio yenye jukumu la kushughulikia masuala ya leseni.
Mhandisi Sementa
amewataka wachimbaji hao kuwa wavumilivu kwani tume ya madini ndo kwanza
imepata uongozi wake hivi karibuni hivyo matakwa yao yatashughulikiwa ndani ya
muda mfupi na kuongeza kwa kuwataka wachimbaji kufuata maelekezo wanayopewa
hasa katika kipindi hiki cha msimu wa mvua
No comments:
Post a Comment