MLELE
Shule ya
msingi kusa iliyopo katika kijiji cha Kanoge kata ya utende Halmashauri ya
wilaya ya Mlele mkoa wa Katavi inatalajia kutatua changamoto ya upungufu wa
madarasa baada ya shilika la elimu Tanzania TEA kudhamini ujenzi .
Akizungumzana MPANDA FM Kaimu Mhandisi wa wilaya hiyo bwana Tano Athuman wazabanga amesema shirika la elimu tanzani TEA limedhamini ujenzi wa miundombinu hiyo ambapo Zaidi ya shilingi 110 zinatarajia kutumika katikaujenzi huo.
Aidha
bwana wazabanga ameeleza mipango mikakati iliyopo katika kupeleka huduma ya
umeme katika shule hiyo
Nae
mwalimu mkuu wa shule hiyo bwana alex Mnyeke ameipongeza halimashauri hiyo kwa
kipaumbele katika ujenzi wa madarasa hayo na kuongeza kuwa itakuwa imetatua
changa moto ya ukosefu wa upungufu wa madarasa.
Source:Paul
mathius
No comments:
Post a Comment