DAR ES SALAAM.
Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania imesema
haina mpango wa kuuza wala kuteketeza meno ya tembo iliyonayo.
Hayo yameelezwa na , katibu mkuu wa Maliasili na
Utalii, Meja Jenerali Gaudence Milanzi ambapo ameutaja uamuzi huo kuwa
utasaidia kupambana na ujangili nchini na Afrika kwa ujumla.
Kwa kutambua uwepo wa zaidi ya tani 118 za meno
hayo nchini ambayo wakati fulani wadau waliishauri Serikali ama kuyauza au
kuyateketeza, katibu mkuu huyo alisema yataendelea kutunzwa.
Kwa mujibu wa makubaliano yaliyoridhiwa mwaka
1975 na mataifa mbalimbali duniani chini ya mkataba unaopiga marufuku biashara
ya wanyama na mimea iliyo hatarini kutoweka (Cites), nchi zote zinapaswa
kuteketeza nyara inazokamata au ilizonazo ili kuvunja nguvu masoko ya vitu
hivyo duniani.
Hazina ya meno hayo iliyopo, Meja Jenerali
Milanzi alisema imetokana na makusanyo yaliyofanywa tangu miaka ya 1960 kutoka
kwa tembo waliokufa, operesheni za kupunguza idadi ya tembo na nyara
zilizokamatwa kutoka kwa majangili.
SOURCE:MOO BLOG
No comments:
Post a Comment