DAR ES SALAAM.
Wamiliki
wa majengo na vyombo vya usafiri na usafirishaji, wafanyabiashara na wananchi
wametakiwa kununua vifaa na mifumo ya kinga na tahadhari dhidi ya moto.
kwa
mawakala waliosajiliwa kuuza vifaa vya zimamoto kwa mujibu wa sheria
Jeshi
la Zimamoto na Uokoaji limetoa rai hiyo leo kupitia taarifa kwa umma iliyotolewa na ofisi
ya habari na elimu kwa umma ya Jeshi hilo.
Taarifa
hiyo imeeleza kuwa, Jeshi hilo halifanyi biashara ya kuuza vifaa vya kuzimia
moto wala kuvifanyia matengenezo pamoja na mifumo ya kinga na tahadhari dhidi
ya moto, bali husimamia na kuhakiki ufungwaji wa vifaa hivyo.
Ukaguzi
hufanyika kwa mujibu wa sheria namba 14 ya mwaka 2007 ikisomwa pamoja na kanuni
ya vyeti na usalama wa moto ya mwaka 2008 na marekebisho ya mwaka 2014 pamoja
na kanuni ya tahadhari dhidi ya moto kwenye majengo ya mwaka 2015.
Source: mwananchi
No comments:
Post a Comment