Waziri wa fedha wa Sudan Bw Mohamed Osman al-Rikabi |
KHARTOUM
Waziri wa fedha wa Sudan Bw Mohamed Osman al-Rikabi amesema uchumi wa Sudan
unakabiliwa na changamoto, lakini zinatatulika kwa sera na utaratibu.
Bw. Al-Rikabi amesema moja kati ya changamoto
hizo ni kushuka kwa thamani ya paundi ya Sudan na kupanda kwa gharama za
kununua bidhaa za kimkakati pia ni suala linalojitokeza.
Pia amesema taabu ya kupata fedha kutokana na
tuhuma kuwa Sudan inafadhili ugaidi na urali wa kibiashara ni changamoto
nyingine inayoikabili Sudan.
Ameongeza kuwa Sudan bado haijanufaika na uamuzi
wa Marekani wa kuiondolea vikwazo mwezi Oktoba mwaka jana, lakini anaona
matokeo mazuri ya uamuzi huo yataonekana baada ya muda.
Chanzo:
Dw swahil
No comments:
Post a Comment