Watu 9 wameuawa usiku wakati makabiliano kati ya waandamanaji na vikosi vya usalama yanaendelea kwa siku ya sita.
Ghasia za hivi karibuni katika eneo la kati kati mwa nchi la Isfaham, zilifikisha idadi ya watu waliouawa kuwa 22.
Waandamanaji sita waliuawa wakati wa kile kilichotajwa kuwa jaribio la kutwaa silaha kutoka kituo cha polisi.
Kwingineko mvulana wa umri wa miaka 11 na mwanamume waliuawa kwenye ghasia akiwemo mwanajeshi wa kikosi cha ulinzi.
Maandamano katika miji kote nchini Iran ndiyo makubwa zaidi tangu ya mwaka 2009 ya uchaguzi wa Urais.
Yalianza Alhamis iliyopita kwenye mji wa Mashhad dhidi ya kupanda kwa bei ya bidhaa na ufisadi na sasa yamesambaa.
Mamia ya watu wamekamatwa.
Rais Hassan Rouhani alisema maandamano hayo ni fursa na wala sio tisho, lakini aliapa kuwachukulia hatua wale wanaovunja sheria.
Marekani imeaunga mkono waandamanaji.
Chanzo:Bbc swahil
No comments:
Post a Comment