Thursday, 18 January 2018

Walimu wa shule za sekondari za binafsi mkoani Katavi wameelezea kuwepo kwa changamoto utekelezaji wa agizo la kuweka kiwango sawa cha ufaulu kwa shule za binafsi na serikali.


MPANDA

Walimu wa shule za sekondari za binafsi mkoani Katavi wameelezea kuwepo kwa  changamoto utekelezaji wa agizo la kuweka kiwango sawa cha ufaulu kwa shule za binafsi na serikali.

Kauli hiyo inakuja kutokana na maagizo ya serikali kupitia wizara ya elimu na mafunzo ya ufundi ambapo shule binafsi zimetakiwa kubadilisha mfumo kwa ufaulu wa wanafunzi na kuwa sawa na shule za serikali.

Wamesema itawalazimu kubadilika japo hatua hiyo haitamjenga mwanafunzi kitaaluma kwani wengi wao wanaosomea katika shule binafsi ni wale walioshindwa kufaulu kwenye shule za serikali.

Hatua hiyo ya wizara ya elimu imetajwa kuwa ni moja ya kupunguza upatikanaji wa wanafunzi watakao jiunga na shule binafsi  kwani kutakuwa hakuna umuhimu kutokana na usawa katika viwango vya ufaulu.

Chanzo:Esther Baraka 

1 comment:

Mwl Sanguapo said...

Mimi naitwa Charles Dionise Sanguapo ni mwalimu wa masomo ya sanyansi ya kilimo na biolojia mwenye cheti ya shahada ya kwanza niliyoipata SUA ikiwa mtapendezwa napenda kufanya uelimishaji wa kilimo ktk kipindi chenu cha kilimo haba na haba

Featured post

MASIKINI WEEE!!!!! KICHANGA CHA SIKU MOJA CHAOKOTWA KATIKA KIWANJA CHA MPIRA AZIMIO

Na;Ezelina Yuda Mtoto mchanga mwenye jinsia ya Kike anayekadiriwa kuwa wa siku 1 ameokotwa akiwa hai kandokando ya uwanja wa azimio  ...