Thursday, 18 January 2018

Walimu 28 wafukuzwa kazi Zanzibar.

Katibu Mkuu kiongozi wa Baraza la Mapinduzi Abdul-Hamid Yahya Mzee


Zanzibar


Jumla ya walimu 28 wamefukuzwa kazi baada ya kugundulika kutumia fedha za Umma  zaidi ya Shilingi milioni mia moja na arobaini ambazo ni fedha za serikali ya Mapindzi ya Zanzibar.
Katibu Mkuu kiongozi wa Baraza la Mapinduzi Abdul-Hamid Yahya Mzee amesema pamoja na kufukuzwa kazi walimu hao pia wanatakiwa kulipa fedha hizo.
Amesema fedha hizo zinatokana na makosa matatu waliyoyafanya walimu baada ya kufanyiwa Uhakiki katika utendaji wa majukumu yao na kugundulika kuwa wanafanya kazi kinyume na utaratibu wa kisheria.
Amesema miongoni mwa makosa yaliogundulika baada ya Uhakiki huo kuwa Baadhi yao  wameshastaafu na wengine hawahudhurii kazini ambapo  walikuwa wakiendelea kupokea mishahara yao jambo ambalo ni kinyume na utaratibu uliowekwa.
Amesema kati ya walimu hao pia kuna baadhi ya walimu wanane ambao ni wagonjwa wa muda mrefu ambapo kati yao watano wanaendelea na Uchunguzi wa kiafya ,wawili waligundulika kuwa Wazima na mmoja ameshastaafishwa kutokana na Ugonjwa wake.
Hata hivyo amesema kuna walimu wengine pia walikuwa wameshastaafu lakini walikuwa wakiendelea kupokea mishahara isiyo ya halali na wengine kuchukuwa likizo bila malipo huku wakiendelea kutumia mishara katika likizo zao na kusababisha serikali kupoteza  fedha katika kipindi chote ambacho walikuwa wakilipwa.
Aidha katibu Yahya ametowa wito kwa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali kuendelea kuwatafuta walimu ambalo hawajapatikana ili waweze kuchukuliwa hatua za kisheria pamoja na kurejesha fedhaa za mishahara walizoingiziwa.
Akizungumzia Wizara ya Afya amesema kumejitokeza kosa moja la upotevu wa Mshahara wa Mfanya kazi wa kigeni ambaye hayupo Ndani ya Nchi lakini Mshahara wake unapokelewa na mtu asiejulikana.
Amesema tayari hatua za kiuchunguzi zinaendelea ili kumbaini mfanya kazi anaejihusisha na upokeaji wa mshahara wa mfanya kazi huo kinyeme na sheria ili fedha hizo ziweze kutumika kwa mahitaji yalikusudiwa.
Yahya amesema kuwa mpaka sasa zaidi ya shilling Milllion 82 na laki mbali zimesha rejeshwa serikalini ambazo wafanya kazi hao waliofukuzwa walitakiwa kuzirejesha. 
Chanzo:Zanzibar24

No comments:

Featured post

MASIKINI WEEE!!!!! KICHANGA CHA SIKU MOJA CHAOKOTWA KATIKA KIWANJA CHA MPIRA AZIMIO

Na;Ezelina Yuda Mtoto mchanga mwenye jinsia ya Kike anayekadiriwa kuwa wa siku 1 ameokotwa akiwa hai kandokando ya uwanja wa azimio  ...