Wednesday, 17 January 2018

Hospitali ya manispaa ya Mpanda mkoani Katavi haina tatizo la upungufu wa damu salama kwa wagonjwa kama ilivyo kuwa hapo awali.


MPANDA

Hospitali ya manispaa ya Mpanda  mkoani Katavi haina tatizo la upungufu wa damu salama kwa wagonjwa kama ilivyo kuwa hapo awali.

Hayo yamebainishwa na mratibu  wa damu salama wa hospitali hiyo Khadija Juma  amabapo amesema kwa mwezi hutumika chupa 350 na inaingiza chupa 400 mpaka 600 hivyo kiwango hicho kinakidhi mahitaji ya wagonjwa.

Aidha amewaomba kujenga tabia ya  kujitolea damu kwa kwa hiari,wakati wote na siku yoyote katika masaa ya kazi.

 Kwa upande wa Wananchi wamlieza suala hilo kuwa na changamoto Lukuki wakitolea mfano wa kuleta ndugu wanne wa kujitolea damu pindi mgonjwa anapo kuwa na tatizo la kuishiwa damu.

Wiki iliyopita Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, akiwa kwenye uzinduzi wa kampeni ya kuchangia damu Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu amezitaka Hospitali na vituo vya Afya nchini kuhakikisha wagonjwa hawauziwi damu.



Chanzo: Neema Manyama

No comments:

Featured post

MASIKINI WEEE!!!!! KICHANGA CHA SIKU MOJA CHAOKOTWA KATIKA KIWANJA CHA MPIRA AZIMIO

Na;Ezelina Yuda Mtoto mchanga mwenye jinsia ya Kike anayekadiriwa kuwa wa siku 1 ameokotwa akiwa hai kandokando ya uwanja wa azimio  ...