Rais John Magufuli ameahidi kuwaongezea wafanyakazi
mishahara kabla hajamaliza kipindi chake cha urais.
Rais Magufuli amesema hayo leo Mei Mosi katika Sikukuu ya
Wafanyakazi iliyoadhimishwa kitaifa, Iringa.
Akizungumza katika Uwanja wa Samora zilimofanyika sherehe
hizo, Rais Magufuli amesema kutokana na changamoto za kimaendeleo
zinazotakiwa kutatuliwa kwa sasa lakini Serikali itahakikisha inampa
mfanyakazi maisha mazuri na nafuu kwa kudhibiti mfumuko wa bei ya bidhaa
nchini.
"Natamani mwaka huu kupandisha mishahara kwa
wafanyakazi lakini kutokana na changamoto zilizopo za kuajiri wafanyakazi
52,000 nitawalipa nini? nikisema natamka kuongeza mishahara, nitazipata
wapi?”amesema Magufuli.
Rais Magufuli amesema iwapo wanataka waongezewe mishahara
labda vyama vya wafanyakazi viuze miradi yao ili wajiongezee mishahara.
No comments:
Post a Comment