Wednesday, 22 November 2017

Mwanachuo mmoja Chuo cha Utumishi wa Umma –Tawi la Tabora kinachojulikana kama Uhazili Raphael Kadesha (22) amefariki dunia baada ya kujinyonga kwa kutumia tai ya kuvaa shingoni.



 
Dkt. Ramadhani Marijani (kushoto)
TABORA.
Mwanachuo mmoja Chuo cha Utumishi wa Umma –Tawi la Tabora kinachojulikana kama Uhazili  Raphael Kadesha (22)  amefariki dunia baada ya kujinyonga kwa kutumia tai ya kuvaa shingoni.

Kwa mujibu wa Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora Graifton Mushi tukio hilo limetokea jana saa 4 asubuhi ambapo marehemu alifunga tai juu ya kitanda chake.

Mushi ameongeza kuwa chanzo cha kifo hicho hakijulikani na Jeshi la Polisi linaendelea na uchunguzi kujua nini kilimfanya mwanachuo huyo kuchukua maamuzi hayo.

Naye Mkurugenzi wa  Chuo hicho Dkt. Ramadhani Marijani ametoa wito kwa wanachuo kuwa watulivu wakati Jeshi la Polisi likiendelea na uchunguzi wa sababu zilizopelekea mwanachuo huyo kuchukua maamuzi yaliyoacha simamazi sio tu kwa familia yake bali hata kwa Jumuiya nzima ya Uhazili.

SOURCES:MPEKUZI.

No comments:

Featured post

MASIKINI WEEE!!!!! KICHANGA CHA SIKU MOJA CHAOKOTWA KATIKA KIWANJA CHA MPIRA AZIMIO

Na;Ezelina Yuda Mtoto mchanga mwenye jinsia ya Kike anayekadiriwa kuwa wa siku 1 ameokotwa akiwa hai kandokando ya uwanja wa azimio  ...