TANGANYIKA
Kijiji cha mchangani kata ya Ikola wilaya ya
Tanganyika inakabiliwa na tatizo la ukosefu wa zahanati hali inayopeleka
kuhatarisha maisha ya wananchi kwani wamekuwa wakitegemea zahanati ya ikola.
Hayo yamesemwa na diwani wa kata ya Ikola
Philenon Mollo katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika kijiji hicho na
kusema kuwa licha ya kijiji hicho kuwa karibu na zahanati ya ikola bado
zahanati hiyo imekuwa ikizidiwa kutokana na ongezeko la watu.
Aidha ametoa wito kwa wananchi kujitoa katika
maendeleo hususani katika kuchangia asilimia 20 ili waweze kuwa na benki ya tofali katika kijiji hicho.
Kwa upande wake mbunge wa mpanda vijijini
Suleiman Kakoso amesema kuwa serikali imetenga kiasi cha shilingi milioni 70
kwa ajili ya kuboresha wodi ya wanawake katika kituo cha afya cha tarafa ya karema ili kuwasaidia wananchi
waliyopo katika tarafa hiyo.
Zahanati ya Ikola iliyopo katika kata ya ikola
wilaya Tanganyika Mkoani Katavi ni
zahanati tegemezi kwa vijiji vyote jirani ikiwemo kijiji cha mchangani,ikola na kafisha.
Chanzo:Restuta Nyondo
No comments:
Post a Comment