Thursday, 15 March 2018

Kamati ya siasa kupitia chama cha mapinduzi mkoani katavi imetoa takribani madawati 15 katika halmashauri tatu.



KATAVI.
Kamati ya siasa kupitia chama cha mapinduzi ccm mkoani katavi imetoa takribani madawati 15 katika halmashauri tatu za mpanda Tanganyika  pamoja na nsimbo.
Madawati hayo yametolewa katika kikao cha Kutoa taarifa ya  utekelezaji wa ilani ya chama hicho kuanzia mwaka 2015 hadi julai mwaka 2017.
Gilbert bagaya akimuwakilisha mkuu wa wilaya ya mpanda liliani matinga katika kikao hicho amesema awamu nyingine kamati hiyo ijikite katika ujenzi wa vyumba vya madarasa kwani  ni tatizo kubwa mkoani katavi.
Mgawanyo wa madawati hayo kila halmashuri huska imepewa madawati 5 kwajili ya  kupeleka katika shule zao yaanze kutumika ambapo madawati hayo yatatumiwa na wanafunzi wapatao 45.
Chanzo: Ester Baraka

No comments:

Featured post

MASIKINI WEEE!!!!! KICHANGA CHA SIKU MOJA CHAOKOTWA KATIKA KIWANJA CHA MPIRA AZIMIO

Na;Ezelina Yuda Mtoto mchanga mwenye jinsia ya Kike anayekadiriwa kuwa wa siku 1 ameokotwa akiwa hai kandokando ya uwanja wa azimio  ...