KATAVI
Wakulima wa zao la Tumbaku
mkoani Katavi wametakiwa kushilikia na
Kampuni ya TLTC inayoshugughulika ununuzi wa zao hilo katika kupanda miti ili
kuhifadhi mazingira kwa manufaa ya kizazi cha sasa na kijacho.
Kauli hiyo imetolewa na Kaimu
meneja wa kampuni ya TLTC Mkoa wa Katavi
Nyabwile Mwakalikene wakati akizungumza na Mpanda redio kuhusu utaratibu
wa wakulima wa tumbaku kupanda miti katika maeneo yao kwaajili ya shughuli ya
kukaushia tumbaku.
Lakini zao la tumbaku limeingia
katika mgogoro mkubwa wa kimasilahi hapa mkoani Katavi kutokana na Serikali ya
mkoa kutangaza mazao mbadala kwa kile
kinacho daiwa kuwa ni kukosekana kwa soko la uhakika.
Mkoa wa katavi nimiongoni mwa
mikoa inayo zalisha kwa wingi zao la Tumbaku ambalo hutajwa kuwa chanzo cha
mapato ya taifa.
Chanzo: Paul Mathias
No comments:
Post a Comment