KATAVI
Viongozi wa Chama cha
ACT-Wazalendo Mkoa wa Katavi wamefika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Katavi Meja
Jeneral Mstaafu Raphael Muhuga kwa ajili ya kutafuta mwafaka wa mazao ya wananchi wa kata hiyo katika maeneo
walio ondolewa yanayo daiwa kuwa hifadhi ya misitu.
Mwenyekiti wa chama
hicho Bw. John Malack akiwa na Katibu wake Bw.Joseph Mona ameeleza kuwa Mkuu wa
Mkoa ameruhusu wakazi wa Kata ya Sitalike kuvuna mazao katika Mashamba yao.
Baadhi ya wananchi wa
kata hiyo ambao wameambatana na ujumbe wa ACT-Wazalendo pamoja na uongozi wa
kata hiyo wamesema wameridhishwa na majibu ya Mkuu wa Mkoa.
Kwa upande wake Mkuu wa
Mkoa wa Katavi Meja Jeneral Mstaafu Raphael Muhuga amekiri kuwaruhusu wakazi
walioondolewa katika makazi yao kuvuna mazao yao huku akisema atapanga ratiba
ya kwenda kufanya Mkutano wa hadhara ili kuzungumza na wananchi.
Wananchi wapatao 3500 wa
vitongoji vya Situbwike,Makutanio na Mgorokani wameathiriwa zaidi na operesheni
hiyo iliyofanyika mwezi agost 2017.
Chanzo: Issack Gerlad
No comments:
Post a Comment