TANGANYIKA
Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika mkoani Katavi Mh Salehe Mbwana Mhando
amewataka Viongozi wa Kata zote za wilaya hiyo, kwa kushirikiana na bodi za
shule kuchukua hatua za haraka kutatua changamoto zilizopo shuleni ili kuinua
kiwango cha elimu.
Mapema leo amefanya ziara kwa shule za Msingi
na shule za sekondari ikiwa na nia ya kukagua maendeleo na uimarishaji wa
miundo mbinu katika shule hizo.
Mkuu wa wilaya ya Tanganyika Mh Salehe Mbwana Mhando aliye kati kati akisindikizwa na walimu wakati wa ukaguzi wa miundo mbinu katika shule ya sekondari Kabungu. |
Miongoni mwa mambo yaliyo jiri katika ziara
hiyo ni pamoja na suala la utoro ambapo ameagiza bodi za shule kwa kushirikiana
na Wazazi na Walezi kuhakikisha wana komesha vitendo hivyo ambavyo amevitaja
kuwa kikwazo cha ukuaji wa elimu katika wilaya hiyo.
Katiki
hatua nyingine ameagiza kukamatwa kwa wazazi wote ambao wanachangia kuwepo kwa
utoro kwa wanafunzi kutokana na kuwatumikisha mashambani.
Wiki
iliyopita wadau wa elimu Mkoani Katavi wamechangia zaidi ya milioni 150
kwaajili ya kuimarisha miundo mbinu ya elimu wilayani Tanganyika.
Chanzo:Rebeca Kija
No comments:
Post a Comment