Mkuu wa wilaya ya Tanganyika Mkoani Katavi Salehe Mhando |
TANGAYIKA
Mkuu wa wilaya ya Tanganyika Mkoani
Katavi Salehe Mhando amesema,vyombo vya ulinzi na usalama wilayani humo vinaendelea
kuwasaka na kuwakamata waharifu mbalimbali wanaohatarisha usalama wa raia na
mali zao ili kuwafikisha katika vyombo vya sheria.
Muhando ametoa kauli hiyo wakati
akizungumza na Mpanda Radio kuhusu utekelezaji wa agizo lake alilolitoa hivi
karibuni akiwataka wanaomiliki silaha kinyume na sheria kuzisalimisha ambapo amesema
silaha tatu zimekamatwa.
Aidha amewataka wananchi kuendelea
kutoa ushiorikiano kwa jeshi la polisi ili kupambana na uharifu unaojitokeza
huku akiwataka wanaomiliki silaha bila kibali halali kuendelea kuzisalimisha
ili kuepuka mkono wa sharia.
Wakazi wilayani Tanganyika wanataja
miongoni mwa matukio yanayotokea mbali na mauaji kuwa ni uporaji wa mali za
raia nyakati za usiku tangu kuanza mwaka 2018.
Januari 22 mwaka huu,mkuu wa Wilaya
Salehe Mhando akiwa ziarani kata ya Kasekese alitoa agizo kwa wanaomiliki
silaha kinyume na sheria kuzisalmisha kabla ya msako kuanza baada ya Februari 4
mwaka huu.
Chanzo:Issack Gerald
No comments:
Post a Comment