Imebainika kuwa Wazazi na Walezi mkoani Katavi ni chanzo cha
uwepo wa ndoa nyingi katika umri mdogo.
Hayo yamebainishwa na mwangalizi na mtetezi wa haki za binadamu kwa mikoa ya
Katavi na Tabora Kusundwa Wamarwa alipokuwa akizungumza na Mpanda radio fm
amesema suala hilo limeshamiri zaidi vijijini.
Aidha ameongeza kusema kuwa upo mpango wa kuendelea kutoa elimu
ya malezi katika ngazi ya familia kwa kushirikiana na jeshi la Polisi kupitia
kitengo cha Dawati la jinsia na watoto pamoja na kamati za vijiji.
Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS)
imesema mkoa wa Katavi ndio unaoongoza kwa kuwa na idadi kubwa ya wasichana
wanaopata mimba wakiwa na umri mdogo kwa asilimia 36.8, mikoa mingine ni Tabora
36.5 na Simiyu 32.1 huku Dar es Salaam ukiwa mwishoni kwa asilimia 12.
#habari na mwandishi wetu alinanuswe Edward
No comments:
Post a Comment