|
Aliyekuwa
waziri wa ulinzi Joao Lourenco |
Chama tawala cha Angola MPLA kimeibuka mshindi wa uchaguzi wa
wabunge, matokeo ya awali ya yameonyesha.
Chama hicho kilipata asilimia 61 ya kura zilizopigwa siku ya
Jumatano , kulingana na tume ya uchaguzi nchini humo.
Chama cha UNITA kilichopata asilimia 27 kimepinga matokeo hayo.
Uchaguzi huo unakamilisha utawala wa rais Jose Eduardo Dos
Santos.
Uchaguzi huo unakamilika siku ya Jumamosi tarehe 26 mwezi Agosti
kutokana na kucheleweshwa kusambazwa kwa makaratasi ya kupigia kura katika
zaidi ya vituo kumi vilivyopo maeneo ya mashamabani.
Hata hivyo chama tawala cha MPLA kimechukua uongozi mkubwa wa
hadi asilimia 10 ya kura zilizohesabiwa.
|
karatasi ya kupigia kura nchini Angola
Ushindi wa MPLA unamaanisha kwamba urais unakabidhiwa aliyekuwa
waziri wa ulinzi Joao Lourenco ambaye aliteuliwa kuwa mrithi wa Dos Santos.
Hatahivyo Dos Santos ambaye utawala wake wa miaka 38 unamweka
kuwa kiongozi wa pili aliyetawala kwa muda mrefu duniani ataendelea kudhibiti
chama hicho.
Siku ya Alhamisi, Chama cha Unita ambacho mgombea wake Isias
Samakuva amkeuwa mpinzani mkuu wa Lourenco, kimesema kuwa kimefanya hesabu yake
ya kura ambapo matokeo yake ni tofauti na yale yaliotolewa na tume ya uchaguzi.
Chini ya mfumo wa kupiga kura wa Angola, raia walitakiwa
kuchagua mgombea na chama chake katika uchaguzi huo.
Chama cha MPLA ndio chama cha kipekee kilichotawala taifa hilo
tangu lilipojipatia uhuru wake kutoka kwa Ureno 1975.
Huku Dos Santos akijiuzulu kama rais, wanawe bado wanashikilia
nafasi muhimu za utawala.
#habari kutoka bbc swahili
|
No comments:
Post a Comment