KATAVI
Jamii imetakiwa kujenga tabia ya kuchangia damu salama kwa ajili ya
kuokoa maisha ya watanzania .
Hayo yamebainishwa na mratibu wa damu salama mkoa wa katavi Hadija Juma
katika kipindi cha kumekucha Tanzania kinachorushwa na mpanda redio katika
uzinduzi wa uchangiaji damu salama utakaofanyika tar 14 mwezi huu katika uwanja
wa shule ya msingi kashato.
Aidha amesema watu wengi katika mkoa
wa katavi hawana tabia ya kwenda kuchangia damu ambazo zinatumika kwa
wagonjwa hali ambayo inasababisha kuongezeka kwa vifo ambavyo vinatokana na
upungufu wa damu salama katika hospitali.
Chanzo:Rebecca Kija
#Changia Damu Okoa Maisha
No comments:
Post a Comment