Thursday, 16 November 2017

Serikali imetoa ruksa kwa Halmashauri nchini kuajiri maafisa watendaji wa kata pale inapoona kunaupungufu.



 

DODOMA

Serikali imetoa ruksa kwa Halmashauri nchini kuajiri maafisa watendaji wa kata pale inapoona kunaupungufu.

Kauli hiyo imetolewa leo Bungeni  na Waziri mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kasimu Majaliwa alipokuwa akijibu maswali yaliyo ulizwa na wabunge mapema leo.

Waziri Mkuu amefafanua kuwa serikali inatambua uwepo wa upungufu wa watumishi wa kada mbali mbali hali iliyosababishwa na zoezi la uhakiki wa watumishi hewa ilikiwemo vyeti feki.

Halmashauri nyingi nchini Tanzania zimekumbwa na tatizo hilo la uhaba wa watumishi jambo linalotajwa kuwa kikwazo katika mstakabali wa maendeleo.

Source: Bunge TV

No comments:

Featured post

MASIKINI WEEE!!!!! KICHANGA CHA SIKU MOJA CHAOKOTWA KATIKA KIWANJA CHA MPIRA AZIMIO

Na;Ezelina Yuda Mtoto mchanga mwenye jinsia ya Kike anayekadiriwa kuwa wa siku 1 ameokotwa akiwa hai kandokando ya uwanja wa azimio  ...